Tuesday, November 20, 2007

Mgeni Rasmi Mzalendo Samueli Sitta, Spika wa Bunge na
Mlezi wa TPN Mzalendo Dr. Maua Daftari, wakifuatilia hafla
Mzalendo Edwin Francis, Managing - Command,
akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo\

Mzalendo Mh. Samuel Sitta, Spika wa Bunge akitoa nasaha
Mzalendo Edwini Francis Mkurugenzi Mwamulishaji wa Kampuni ya
Fulltime Security Services akipokea tuzo kutoka kwa Mzalendo Spika


Viongozi wa TPN wakijadiliana jambo


Mtandao wa Wanataaluma na Wasomi Tanzania (Tanzania Professionals Network – TPN), ulifanya Hafla ya Kutunisha Mfuko wa Ujasiliamali na Uwezeshaji wa Kiuchumi. Hafla hiyo ilifanyika, Jumapili Tarehe 18 Novemba 2007, Viwanja vya Karimjee, Kuanzia saa 10.00 Jioni. Mh. Samuel Sitta, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano alikuwa Mgeni Rasmi.

Katika Hafla hiyo TPN iliandikisha wanachama wapya. Pia katika hafla hiyo TPN iliwatambua na Kuwatunukia makampuni mawili ya Wanataaluma Wajasiliamali na Mwanataaluma mmoja Mwajiriwa ambao wamekuwa ni mfano wa kuigwa kwa Wanataaluma wengine.

Emec Engineering Limited (www.emec.co.tz) na Fulltime Security Services Limited (www.fulltimesecurity.net) walitunukiwa vyeti na tuzo ta Wajasiliamali Wanataaluma Waliofanya vizuri. Walianzisha kampuni zao miaka michache iliyopita bila mitaji wala mjomba au benki ya kuwasaidia fedha. Walianza kwa taabu sana. Lakini kwa Ujasiliamali wao waliweza kuonyesha bidii kubwa na leo Makampuni yao ni mmoja ya Makampuni Makubwa Sana yanayoheshimiwa kiasi cha kuwa tishio kwa makampuni makongwe nay a kigeni.

Pia Mkurugenzi Mwendeshaji wa the Foundation Society Mr. John Ulanga alitunukiwa cheti na tuzo ya kuwa Mwanataaluma bora wa kuigwa katika utendaji wa kazi. Akiwa kiongozi, amefanikiwa kuendesha organization ambayo imeshatoa misaada katika miradi zaidi ya 700 toka mwaka 2003 yenye thamani zaidi ya TZS Billion 18. Amekataa katakata kufanya kazi kwa mtindo wa kutokuwa Muadilifu. Ilibidi kipindi Fulani asimamishwe kazi kwa tabia yake ya uadilifu wa kupita kiasi. Hata hivyo baada ya ukweli wa fitina kujulikana ilibidi bodi yote ijiuzulu na kumfanya Mwanataaluma John Ulanga kuanza kupanga safu mpya ya maafisa wake baada ya wababaishaji kutimuliwa. (www.thefoundation-tz.org).

Big up Wanataaluma mliopata tuzo. Kazeni Buti (Kwa msemo wa vijana wetu wa mjini)

Katika hafla hiyo iliyohusisha viongozi wa taasisi mbalimbali, wizara, wanataaluma, wafanyabiashara na wanataaluma wengi, Takribani Million 30 Zilipatikana ikiwa ni ahadi na makusanyo.

Baadhi ya matukio yaliyovutia ilikuwa ni mnada wa vitu mbalimbali. Katika baadhi ya vitu:
· Picha ya Raisi Kikwete ilinunuliwa kwa Shs Million 1
· Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Shs 1 Million
· Picha ya Spika TZS Laki 3
· Pen ya Spika (Gold Plated) ambayo aliitumia kusaini Wakati akiapishwa kuwa Spika TZS 1.5 Million
· Na Tai ambayo Spika aliivua na kuitoa kwa Mnada TZS Laki 5.

Kwa habari zaidi, tembelea tovuti ya TPN: www.tpn.co.tz; NB: Registration kupitia tovuti ya TPN bado haifanyi kazi

Blog: www.tpn-tz.blogspot.com; Kujiunga na TPN, tuma barua pepe register@tpn.co.tz

Kujiandikisha uanachama ni TZS 100,000.00 na Ada ya Kila Mwezi ji TZS 20,000.00. Tuma maombi na utaletewa fomu maalumu ya kujiunga rasmi. Kila mwanachama hai kwa sasa lazima ajiandikishe na kulipia ada.

Be Prepared for the true Mentorship and Inspirational Seminar – No blabla, no politics. This is Special for New Year
Date: Thursday 10th January 2008
Dinner will be served.
Details will be provided later.

0 Comments:

Post a Comment



 

FREE HOT VIDEO | HOT GIRL GALERRY